JOPO LA KISWAHILI

Wanajopo wamejitolea kwa kila hali kuhakikisha kuwa lugha imeimarika hasa nyakati hizi ambapo kuna athari ya lugha sheng’.

Shule imefanya ima fa ima kuhakikisha Kiswahili kinafundishwa na walimu wenye tajriba pana. Aidha, jopo zima limeimarika zaidi kwa kuwapo kwa waandishi wa vitabu bora vinavyotumika nchini kufunzia Kiswahili. Mathalani Kurunzi ya marejeleo Halahala, Kurunzi ya Insh, Tadubiri ya Insha miongoni mwa vingine. Vivyo hivyo silabasi huzingatiwa kwa kina.

Ili kuwapa wanafunzi mshawasha na ujasiri wa kuzungumza, kusoma na kuandika Kiswahili tunawashirikisha na kuwahusisha katika;

  • Mashairi, nyimbo na midahalo
  • Tumeunda kitengo cha wanahabari chipukizi
  • Kuwapa nafasi kuchangia katika vipindi vya Kiswahili vanavyopeperushwa moja kwa moja kwenye redio na runinga

Alhasili shule imeandikisha matokeo ya kuhusudiwa katika somo hili kwa miaka memgi.

  • Kwa kuwa lugha ni bahari, wanafunzi na walimu wameamua kufanya utafiti jari moja kwa matokeo aula siku za usoni.
  • Katika jopo hili, mwanafunzi amepewa kipaumbele. Kufaulu kwa mwanafunzi ndiyo shabaha yetu.
  • Siku ya kuzungumza Kiswahili.